Saturday 5 April 2014

SAUT-SEMA WASHIRIKI KATIKA PROGRAM YA USAFI JIJI LA MWANZA

Jiji la  Mwanza linaongoza kwa usafi kuliko majiji yote hapa Tanzania.Ukifika Mwanza utajionea ni jinsi gani utaratibu wa usafi unavyotekelezwa hususani maeneo yanokaliwa na watu na maeneo ya biashara kama, soko, stand na kandokando ya barabara.


HALMASHSAURI YA JIJI LA MWANZA IMEJIWEKEA UTARATIBU WA KUFANYA USAFI MAENEO YOTE YA JIJI KILA JUMAMOSI YA KWANZA YA MWEZI. MWEZI HUU WA APRILI UONGOZI WA MKOA WA MWANZA NA HALMASHAURI YA JIJI ILITEKELEZA PROGRAM YA USAFI KATIKA KATA ZA MKOLANI NA BUTIMBA HASWA ENEO LA STAND KUU YA NYEGEZI.
PATA HABARI KWA PICHA:

MKUU WA MKOA WA MWANZA ENG. EVARIST WELLE NDIKILO (KULIA) NA MKUU WA WILAYA YA NYAMAGANA MH. BARAKA KONISAGA, WAKIWA TAYARI KUTEKELEZA PROGRAM YA USAFI NDANI YA STAND YA NYEGEZI


Rais wa SAUTSO ndg Philbert Saimon (mwenye suti nyeusi ) na Mwenyekeiti wa SAUT-SEMA Ndugu Katalyeba wa kwanza kushoto na Afisa Habari wa Saut-SEMA ndugu Ngogo Mang'enyi wa pili kushoto, wakiwa tayari na wanamazingira ndani ya stand ya mabus Nyegezi kwa ajili ya kuanza shughuli ya mazingira



Mstahiki Mayor wa jiji la Jiji la Mwanza Mh. Stansalaus Mabula ambaye ni diwani wa kata ya Mkolani naye alishiriki kikamilifu




Diwani wa kata ya Butimba Mh. Dismas Masanu (kulia) na Mkurugenzi wa jiji la mwanza ndugu Hida Alphahazan wakiwa tayari kufanya usafi


KAZI ILIANZA HIVI: HILI JENGO NI MAARUFU SANA KWA KULAZA WASAFIRI WANAO ENDA MIKOANI PIA HUMUHUMU MAMA NTILIE HUFANYA SHUGHULI ZAO ZA KILA SIKU ZA KUANDAA CHAKULA KWA WATEJA WAO. HAPO NDIPO SHUGHULI ILIANZIA KWA KUONDOA MAGODORO YOTE NA KUSAFISHA ENEO HILO

.
 MAGODORO HAYO YAKAKUSANYWA KATIKA ENEO LA KUKUSANYIA TAKA 
KISHA  KUYATEKETEZA KABISA.

Ndege huyu hujulikana kama The Marabou Stork (Leptoptilos crumeniferus) maranyingi hupatikana maeneo yenye uvundo na uchafu wa muda mrefu na hapa Nyegezi ndo waliotawala eneo hili kutokana na mrundikano wa uchafu katika eneo la stand ya mabus la Nyegezi.

Wana SAUT-SEMA walihakikisha hakuna uchafu unaozagaa katika eneo zima la Nyegezi stand walizibua mitaro na kupeleka taka mahala panapo husika

 Baada ya kazi wanaSAUT-SEMA wakapata picha ya pamoja
Sehemu ya wananchi walioshiriki katika program ya usafi katika jiji la Mwanza eneo la Nyegezi stand

RAIS WA SAUTSO NDUGU PHILBERT SAIMON AKITOA NENO LA SHUKURANI KWA UONGOZI WA MKOA WA MWANZA NA JIJI LA MWANZA KWA KUFANIKISHA PROGRAM YA USAFI'

MWENYEKITI WA SAUT-SEMA NDUGU TIBEZUKA KATALYEBA  NAE AKAPATA NAFASI YA KUSHUKURU

MWISHO MKUU WA MKOA WA MWANZA NDUGU EVARIST WELLE NDIKILO AKAHITIMISHA ZOEZI ZIMA KWA KUWAHUTUBIA WANANCHI WALIOFIKA KUSHIRIKI ZOEZI ZIMA LA USAFI
KISHA KILA MMOJA AKAANZA SAFARI YA KURUDI MAJUMBANI



IMEANDALIWA NA IDARA YA HABARI NA MAWASILIANO
SAT-SEMA
MWANZA
TX
NGOGO MANG'ENYI
THE SAUT-SEMA IT AND TECH OFFICER






Siku ya mazingira duniani

SAUT-SEMA Life prosperity depends on Environment Siku ya mazingira duniani