Siku ya Kimataifa ya Uhifadhi wa Tabaka la Ozoni | 16 Septemba
Tabaka ambalo hulinda Dunia kutokana na sehemu yenye madhara ya miale ya jua, hivyo kusaidia kuhifadhi uhai kwenye sayari. Kukomeshwa kwa matumizi yaliyodhibitiwa ya vitu vinavyoharibu ozoni na upunguzaji unaohusiana na hivyo sio tu umesaidia kulinda tabaka la ozoni kwa kizazi hiki na kijacho, lakini pia kumechangia kwa kiasi kikubwa juhudi za kimataifa za kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa; zaidi ya hayo, imelinda afya ya binadamu na mifumo ya ikolojia kwa kuzuia mionzi hatari ya urujuanimno kufika Duniani.
Kihistoria Kemikali kadhaa zinazotumiwa sana zimegunduliwa kuwa zinaharibu sana tabaka la ozoni. Ikiwemo Halokaboni ambayo atomi moja au zaidi za kaboni huunganishwa na atomi moja au zaidi ya halojeni (florini, klorini, bromini au iodini). Aidha Halokaboni zilizo na bromini kawaida huwa na uwezo wa juu zaidi wa kuharibu ozoni (ODP) kuliko zile zilizo na klorini.
Kemikali zinazotengenezwa na binadamu ambazo zimetoa zaidi klorini na bromini kwa uharibifu wa ozoni ambayo kikawaida methyl bromidi, methyl kloroform, tetrakloridi kaboni na familia za kemikali zinazojulikana kama haloni, klorofluorocarbons (CFCs) na hidroklorofluorocarbons (HCFCs).
Mnamo 1994, Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa lilitangaza tarehe 16 Septemba Siku ya Kimataifa ya Uhifadhi wa Tabaka la Ozoni, kukumbuka tarehe ya kutiwa saini, mnamo 1987, Itifaki ya Montreal juu ya Vitu Vinavyopunguza Tabaka la Ozoni (azimio 49/114).
Tuna Kila sababu ya kutunza mazingira yetu kwani uhalisia wa uhai hutegemea uwepo wa uoto bila kusahau utunzaji Bora wa Tabaka la Ozon tuungane Kwa pamoja katika kuazimisha siku hii Duniani
Tembelea kurasa zetu kupitia facebook na instagram kama sautsena na vilevile twitter kama sautsema1
Imetolewa na ICT SAUTSEMA
Raphael Msukuma
SAUTSEMA
life prosperity depends on the Environmrnt
No comments:
Post a Comment